-->

Wema Sepetu: Mimi ni Kama Dhahabu

MREMBO wa filamu Tanzania, Wema  Sepetu, amesema yeye ni dhahabu inayogombewa na watu hivyo hajali hata kama atachafuliwa namna gani katika mitandao ya kijamii.

WEMA SEPETU298

Wema aliliambia MTANZANIA kwamba, hana mpango wa kujibu vibaya vinavyoongelewa kuhusu yeye kwa kuwa yeye bado ni dhahabu inayotamaniwa kushikwa na kila mtu.

“Mimi ni kama dhahabu hivyo kila mtu anatamani kuishika, watu wanaacha kufanya yao kila siku Wema,  kwa sasa niko na mambo yangu ya kutafuta fedha sina habari na mtu hata aniandike vibaya vipi,” alisema Wema.

Aliongeza kwamba licha ya kusemwa, amezidi kujiongezea mashabiki na mikataba mbalimbali ya kufanya kazi na makampuni yenye majina makubwa kwa kuwa yeye ni kama dhahabu isiyochafuka.

Mtanzania

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364