MWIGIZAJI wa filamu za Bongo, Wema Sepetu, amewaomba radhi watu wote aliowahi kuwakosea na amesema amewasamehe wote waliomkosea.
Wema alisema kwa sasa ameelekeza ibada yake mwezi huu mtukufu wa Ramadhani ili kusudio alilojiwekea kabla ya mfungo huu litimie.
“Ninaamini kabisa ibada yangu ninayoifanya hadi usiku itapokelewa vyema na itafanikisha azma yangu na kuondoa makandokando na majina yote ya ajabu wanayoniita wasionitakia mema,” alisema Wema.
Wema aliongeza kwamba pia amechoshwa na tabia za watu wanaomhisia vitu vya ajabu ambavyo hajavifanya, vitu ambavyo hakuwa tayari kuvitaja huku akisisitiza kwamba imani yake kubwa kipindi hiki cha mfungo na ibada anazofanya zitawafedhehesha wenye nia mbaya naye.
Mtanzania
Comments
comments