Wema Sepetu: Siwezi Kuvunja Kiapo cha Kufunga Kizazi
WEMA Isaac Sepetu amefunguka kuwa, kamwe hawezi kuvunja kiapo alichoweka kuwa akitimiza umri wa miaka 30 bila kupata mtoto atafunga kizazi.
Wema aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa, kuwa alitoa ahadi kuwa atakapofikisha umri wa miaka 30 bila kunasa ujauzito, basi atafunga kizazi na kwenda kuasili mtoto.
“Mwaka ndiyo hivyo unaisha, lakini ahadi yangu iko palepale. Kama kweli sitanasa ujauzito hadi nagonga miaka 30 kamili, lazima nifanye nilivyoahaidi na nitaenda kuasili mtoto,” alisema Wema ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 29.
Chanzo:GPL