Kundi la Weusi limedai kuwa na mipango ya kutengeneza studio yao pamoja na kujenga ofisi.
Wakiongea na Planet Bongo ya East Africa TV baadhi ya wasanii wanaounda kundi hilo akiwemo Nick wa Pili, Joh Makini na G-Nako wamesema kuwa wapo kwenye mipango ya kutengeneza studio yao na ofisi kwa pamoja.
“Tuna mpango wa kuwa na studio pamoja na ofisi. Hii ndiyo mipango ya mwaka huu na mwakani,” amesema Nick wa Pili kwa niaba ya Weusi.
Mpaka sasa kundi hilo limeshafanikiwa kuachia nyimbo pamoja ukiwemo ‘Gere’ huku mara nyingi kila msanii akifanya kazi zake binafsi.
Bongo5
Comments
comments