Wolper Afunguka kuachana na Brown
Msanii Jackline Wolper ambaye hivi karibuni amekumbwa na tetesi za kuachana na mpenzi wake, amekanusha taarifa hizo na kusema kwamba wakiachana mashabiki wake watajulishwa.
“Watanzania wamezoea sana Instagram, usipompost bwana wako basi mmeachana, hawajui hata kama watu mumepata deal, mmeingia mikataba, hautakiwi kuweka mapicha ya mapenzi, mpaka wanataka utoe siri sasa, kuna issue siwezi kuiongelea, hivyo hakuna kitu kama hicho kikiwepo nitaongea”, amesema Wolper
Wolper amekutwa na tetesi za kuachana na Brown baada ya kuonekana akishikana mkono kusalimiana na x wake, kwenye sherehe ambayo wawili hao walihudhuria.