Mwanadada mwanamitindo na mwigizaji maarufu nchini, jackline Wolper Massawe ametangaza makubwa ujio wa ndoa yake inayotarajiwa kufanyika hivi karibuni mara baada ya kuwa tayari ameshatolewa mahali.
Wolper amedai kuwa ndoa hiyo inatarajia kugharimu kiasi cha shilingi milioni 60 za kitanzania, ikiwa milioni 50 kutumika kwa ajili ya harusi itayofanyika Dar huku milioni 10 kutumika harusi itayofanyika Marekani.
“Milioni kama 50 zitatumika kwenye sherehe ya hapa Bongo na nyingine 10 nje kwa sababu kule Marekani hatutakuwa na watu wengi sana,” alisema Wolper.
Akizungumza hayo pindi alipohojiwa na moja ya chombo cha habari mjini , Wolper amesema kuwa kwenye harusi inayotarajiwa kufanyika Marekani anatarajia kusindikizwa na wasanii wanne akiwepo Anty Ezekiel, huku wengine watatu bado hawajajulikana kwa majina yao.
‘’Wasanii ambao nitaenda nao kwa ajili ya kuhudhuria harusi yangu ni wanne tu, mmoja kati yao ni Aunt Ezekiel kwa sababu huwa ananipa sapoti kwenye biashara zangu hivyo siwezi kumwacha,” alisema Wolper
Wolper amesema kuwa gharama zote za wasanii watao msindikiza zitaakuwa juu yake yaani kuanzia usafiri wa hapa nchini hadi pesa yao ya kujikimu pindi wawapo nchini Marekani.
Comments
comments