Artists News in Tanzania

Wolper Arejea CCM

WOLPER (5)

Wolper akitangaza sababu za kurejea CCM.

Wolper akiongea na Mwenyekiti Mstaafu Mhe. Jakaya Kikwete.

Wolper akiongea wakati wa hafla ya wasanii ya kumuaga Mwenyekiti Mstaafu Mhe. Jakaya Kikwete.

Na Leonard Msigwa/GPL

MWANADADA gumzo kwenye tansia ya Bongo Movie nchini, Jacqueline Wolper hatimaye jana ametangaza rasmi kurejea Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Wolper ambaye alikuwa kada wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na mfuasi mkubwa wa aliyekuwa mgombea urais wa chama hicho na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Ngoyai Lowassa alitangaza uamuzi huo wakati wa hafla ya wasanii ya kumuaga Mwenyekiti Mstaafu Mhe. Jakaya Kikwete mjini Dodoma.

Baada ya kupewa nafasi kuongea, Wolper alikuwa na haya; “Nilipotea kwenda kule, nimeamua kurudi nyumbani”
Ikumbukwe kwamba Wolper alikuwa mstari wa mbele miongoni mwa wasanii wa kike nchini kumpigia debe bila kificho Edward Lowassa wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka jana na alienda mbali zaidi kwa kumwita Edward Lowassa kama baba yake.

Chanzo:GPL

Comments

comments

Exit mobile version