-->

Young Dee awazungumzia Young Killer, Dogo Janja kuhusu kumchana

Rapa Young Dee amefunguka mambo kadhaa kuhusu Young Killer na Dogo Janja kumchana mara kwa mara kwenye ngoma zao.

Rapa Young Dee

Young Dee amekiambia kipindi cha The Play List cha Times Fm kuwa wasanii hao ni umri tu wanapitia kwa sasa ambao yeye ameshapita huko hivyo hawashangai.

Kuhusu line ya Dogo Janja iliyopo katika wimbo wake wa ‘My Life’ isemayo, “nyie mayoung hamniwezi’, Young Dee alisema amekuwa akifuatilia nyimbo kama hizo kwa muda mrefu na sio hiyo tu kuna nyimbo karibia sita na nyingine zipo studio hazijatoka.

“Huu wimbo My Life maana yake maisha yangu, kama naimba wimbo unaohusu maisha yangu siwezi kumzungumzia mtu mwingine, wimbo ni mzuri lakini hiyo part imekuwa kama imetoka nje ya mada.

“Hata kama wewe ni mkali fanya mambo yako achana na mtu mwingine, simple like that, siwezi kusema mimi ni mkali eti wewe Fid Q huniwezi, hilo hamna kama wewe ni mkali fanya ukali wako,” alisema Young Dee na kuongeza.

“Ni kama shambulio la moja kwa moja lakini huwezi kujua mtu anafanya hiyo kwa lengo gani, mwingine anatafuta publicity, kwa hiyo mimi nitavyoreact ndio itafanya hiyo point ionekane ina make sense au sivyo,” alisema.

Pia aliuchambua line ya Young Killer katika wimbo wa Sinaga Swagga isemayo, “kuhusu kufunikwa siwazi, kuhusu Janjaro na Young Dee mimi ndio mkubwa wao wa kazi,”.

Kuhusu line hiyo Young Dee alisema anajua wanakuwa na itafika point wataacha hayo mambo na kuamua kufanya kazi, lakini sasa hawajaamua kufanya kazi bado wapo kwenye vilinge.

“Na mimi ninapenda kwa sababu wenye wanajua kabla hawajatoka mimi ndiye nilikuwa nawapromote, huyo Young Killer nimempigia simu mimi nikiwa na Belle 9 nakamuhamasisha baada ya kumsikia kwenye kipindi cha Fid Friday Free Style.

“Dogo Janja kabla hajaingia Tip Top, pale Tongwe nilimwambia J Murder.mchukue huyu dogo anachana sana. Lakini siwezi kuwajudge kwa sababu ni umri wanaopitia ambao hata mimi nilipitia,” alisema Young Dee.

By Peter Akaro

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364