Muigizaji wa filamu za bongo Yusuph Mlela leo amezungumza na kumtaka msanii wa muziki wa hip hop na Bongo fleva Nay wa Mitego, kuheshimu na kutoziingilia kazi za wasanii wengine kama anavyoheshimu kazi zake.
Yusuf Mlela aliendelea kwa kusema kuwa kama Nay wa Mitego anaona ameshafanikiwa kimaisha basi awapishe wasanii wengine waendelee kujitafutia riziki kwani bado wana safari ndefu kimaisha.
‘Mimi namuomba sana Nay ajiheshimu sana, asiingilie kazi za watu ambazo hazimuhusu. Kama yeye ameshajiweza kwenye suala la kipato basi akae pembeni atuache wengine tutafute riziki”– alisema Mlela.
Aidha Mlela alizungumzia suala la yeye kutaka pambano la ndoni kati yake na Nay, na kusisitiza ili kurudisha heshima kati ya wawili hao basi ni vyema wakapanda ulingoni na kuzichapa.
“Sawa mimi na yeye tunaweza tukawa hatulingani labda kiuwezo na kimaisha kwa sababu yeye anaona tayari amekwisha rizika, ndio maana namuomba tupande ulingoni ili tuheshimiane. Mimi kama ningekuwa naimba ningeingia studio nikatengeneza wimbo wa kumchana lakini kwa vile kazi zetu haziingiliani ndiyo maana nasisitiza ki Hip hop tuu tuingie ulingoni ili heshima iwepo tuache maneno maneno” alisisitiza Mlela.
Comments
comments