Zari Bado Mbichi Kama Embe la Msimu – Diamond
Wakati kuna watu wanaodhani kwa kuwa ni mama wa watoto wanne, Zari anaweza kuwa ameshapoteza sifa za ‘usichana’, Diamond ana mtazamo tofauti.
Hitmaker huyo wa ‘Utanipenda’ anamuona Zari the Bosslady kama msichana mbichi ma hauchoki uzuri wake.
“I swear I can’t get use to your Cuteness…Kadada kabichiii… kama Embe la Msimu,” aliandika Diamond kwenye picha ya mama huyo wa mtoto wake Tiffah.
Mama Tiffah yupo Dar es Salaam kwa siku kadhaa na ametumia fursa hiyo kumsaidia mumewe kupanga mikakati mipya ya WCB.
“Calling shots…. late night strategic planning. All we see is dollar signs at the WCB Empire,” aliandika Zari.
Chanzo:Bongo5