Zari The Boss Lady Alitambua Kitambo Usaliti wa Diamond Platnumz
UHUSIANO imara wa staa wa muziki wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’ umeanza kulega lega baada ya kutikiswa vibaya na mwanamitindo, Hamisa Mobetto.
Kapo hiyo yenye wafuasi wengi Afrika Mashariki imefanya mambo lukuki ya maendeleo, siyo kwenye mapenzi tu bali uhusiano wao umeingia mpaka katika kazi na kufanya uwe imara zaidi kwenye vita mbalimbali wanazozipitia kutoka kwa makundi kadha wa kadha yasiyopenda uhusiano huo.
Umoja wao katika kazi umefanya wafanye matangazo ya kampuni kadhaa za samani na nguo pamoja na kuwekeza kwenye ardhi kwa kujenga nyumba maeneo ya Madale, Dar es salaam na nchini Afrika Kusini wakanunua jumba la kifahari kwa ajili ya watoto wao, Tiffah na Nillan.
Diamond Platnumz amekuwa akipata kashfa za kutoka kimapenzi na warembo mbalimbali akiwa bado kwenye uhusiano imara na Zari lakini tetesi hizo hakuna aliyewahi kuzithibitisha kwani yeye mwenyewe amekuwa akikanusha vikali na kusisitiza mahapa yake yapo kwa mama watoto wake (Zari The Boss Lady).
Mwanamitindo Hamisa Mobetto naye amekuwa akihusishwa kuchepuka na Diamond mara baada ya kushiriki kama video vixen kwenye video ya Salome iliyotoka mwaka jana. Skendo hiyo imemzidi nguvu Diamond mpaka amekubali kudondoka kitandani na modo huyo mpaka akampa ujauzito wa mtoto wake wa tatu anayeitwa, Dylan.
ZARI ANUSA KUSALITIWA
Kama unafuatilia vizuri utakuwa umewahi kuona tangazo moja la duka la vitu vya nyumbani ambapo mwisho linaonyesha Zari ameziona hereni za kike kwenye kitanda cha Diamond Platnumz. Ubunifu wa tangazo lile ulitokana na tetesi za kweli ambazo Zari aliwahi kuzisema kwenye Snapchat kuwa amekuta herein za bei rahisi kwenye kitanda anacholala yeye na baba watoto wake (Diamond) nyumbani kwao Madale.
Ukiacha hiyo, Juni 13 mwaka huu, Diamond aliandika kwa hasira maneno yanayosema: Ndiyo maana wakati mwingine naonaga bora nile tu na kusepa maana hawathamanikagi wala kuaminika hawa..
Diamond aliandika maneno hayo ya hasira baada ya kuona picha ya Zari akiwa kwenye bwawa la kuogelea akiwa na mwanamume ambaye hamjui. Diamond alijuta kuwekeza kwa Zari maana tayari aliona mzazi mwenzake huyo anafanya usaliti.
Lakini Diamond kwa aibu aliifuta picha ya Zari na hayo maneno baada ya Zari kuitolea ufafanuzi picha hiyo kuwa yule mwanamume aliyekuwa naye kwenye bwawa la kuogelea ni binamu wa aliyekuwa mume wake wa zamani marehemu Ivan Ssemwanga (The Don) anayeitwa Edwin Lutaaya na eneo hilo alikuwa na mke wake ambaye ndiye aliyepiga picha ile.
ALIVYOHISI KUSALITIWA
Katika kutoa ufafanuzi zaidi, Zari aliandika ujumbe ambao yalionyesha Diamond Platnumz anadhani tabia yake ya usaliti na yeye (Zari) anayo ndiyo maana aliandika maneno ya kumkashfu bila hata kumpigia simu kumuuliza kulikoni.
Zari aliandika hivi kwa Kingereza: When you are that IT loyal gal, someone will always find fault when it’s not there just to cover and turn around stories of all the dirty the do behind you back.
DIAMOND PLATNUMZ AMZUGA ZARI KENYA
Chibu alifahamu kuwa tayari amempa ujauzito Hamisa na inawekekana mpenzi wake Zari akagundua, ndipo alipokwenda naye kwenye msiba wa mkwe wake (Mama Zari) nchini Uganda na baada ya mazishi akamchukua na kumpeleka Mombasa, Kenya kumliwaza.
Huku Bongo mambo yalizidi kuharibika kwani Hamisa Mobetto alianza kuonyesha kwenye mitandao ya kijamii kuwa ujauzito wake ni wa Diamond Platnumz na mitandao ikazidi kuchafuka pale ambapo Dylan alizaliwa kwani mwanamitindo huyo alimwita mwanawe jina la baba mzazi wa Diamond (Abdul Juma).
ANARUDI VIPI KWA ZARI?
Zari yupo Afrika Kusini akiendelea kuwalea watoto wake Tiffah na Nillan, Diamond anaona soo kumfuata mrembo huyo ambaye inaonyesha wazi anampenda licha ya mapunguzfu ya kibinadamu yaliyozaa usaliti ili amuombe radhi na masiaha yaendelee.
Japo anasema yupo tayari kutembea na magto toka Bongo mpaka Sauzi ili mrembo huyo wa Kiganda ampe tena nafasi.
NA CHRISTOPHER MSEKENA
Mtanzania